ASANTE KWASI AMTEGA PIERRE

NA TIMA SIKILO

HUENDA beki wa Simba, Asante Kwasi, akamweka mtegoni kocha wake mpya, Pierre Lechantre, katika mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa Jumapili hii dhidi ya Majimaji, katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Mtego huo utakaomkumba Pierre utatokana na beki huyo wa Ghana kuwa na majeraha madogo na kushindwa kufanya mazoezi na wenzake na kujifua peke yake kwa mazoezi mepesi, huku akisema ana uhakika wa kupata namba, kwa kuwa majeraha hayo si ya kumfanya ashindwe kucheza.

Juzi katika Uwanja wa Bandari, uliopo Temeke, ambako kikosi cha Simba kinafanya mazoezi yake, BINGWA lilishuhudia beki huyo, Kwasi na Jjuuko Murshid wakifanya mazoezi mepesi tofauti na wachezaji wengine.

Lakini Kwasi aliliambia BINGWA jana kuwa, alifanya mazoezi mepesi kwa kuwa alikuwa na maumivu kwenye mguu, lakini anaamini atakuwa poa na kama kocha na daktari wataruhusu acheze atakuwa tayari.

“Nina majeraha ya mguu, lakini nina uhakika nitakuwa poa kabla ya mchezo wetu dhidi ya Majimaji kama Mungu akijaalia, hivyo kocha na daktari wakiona hali yangu inaruhusu kucheza nitacheza,” alisema Kwasi.

Kwasi ni mmoja wa wachezaji ambao wanaongoza kwa mabao msimu huu wa Ligi Kuu, ambaye anashika nafasi ya tano, akiwa na mabao sita.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*