KUMBE SALAH ANAWAWAHI URUGUAY BWANA

CAIRO, Misri

SHIRIKISHO la Soka la Misri limetangaza (EFA), imetangaza kuwa fowadi wa timu hiyo, Mohamed Salah, atacheza katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Uruguay.

Kwa mujibu wa Rais wa EFA, Khaled Latif, alisema Salah atakuwepo uwanjani siku hiyo na akaongeza kuwa mashabiki eflfu 40 wa Misri watashuhudia mazoezi ya kikosi hicho yanayomalizika leo katika Uwanja wa Taifa wa Cairos.

“Hata kama hataanza, atacheza dakika chache atakazopangwa,” alidai Latif akizungumza kupitia kituo kimoja cha redio cha Misri.

“Tuna mkutano na EFA, kujadili maandalizi ya mwisho ya mazoezi kabla ya timu haijasafiri kwenda Urusi,” aliongeza.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*