Kompany apewa ‘shavu’ Ubelgiji

BRUSSELS, Ubelgiji

 STAA Vincent Kompany ameteuliwa kuwa kocha mchezaji wa klabu ya  Anderlecht  ya Ubelgiji, baada ya kumaliza kuitumikia Manchester City kwa kipindi cha miaka 11.

Ilitangazwa jana kwamba, Kompany ataondoka klabuni hapo kwa mabingwa wa Ligi Kuu England, baada ya Mbelgiji huyo kumaliza kibarua chake akiiwezesha timu hiyo kutwaa taji la tatu msimu huu.

Kufuatia hali hiyo, kwa sasa hatua nyingine kwa staa huyo mwenye umri wa miaka  33, atarejea nyumbani  Anderlecht,ambako ndiko alikoanzia kabarua chake baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu kama kocha na mchezaji na kwamba kocha wake, Pep Guardiola, amekubali uamuzi wake wa kwenda kujiunga na klabu hiyo ili aweze kurejesha mapenzi yake katika soka.

“Mwisho wa msimu huu utakuwa ni wa kukumbukwa. Nimetimiza ndoto zangu nikiwa na timu hii,” aliandika Kompany katika ukurasa wake wa  Facebook.

“Katika kipindi cha miaka mitatu, nimejifunza mengi nikiwa chini ya kocha mahiri, Pep Guardiola, amerejesha mapenzi yangu katika soka,” aliongeza staa huyo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*