Kolabo ya Weusi, Sauti Sol ni zaidi ya Gere

NA CHRISTOPHER MSEKENA,

BAADA ya kutikisa chati za muziki Afrika kupitia wimbo wao unaoitwa Gere, kundi la Weusi, linaloundwa Joh Makini, Nikki wa Pili na G Nako, limewataka mashabiki wake kukaa tayari kwa ujio wa ngoma yao mpya waliyowashirikisha Sauti Sol kutoka Kenya.

Alizungumza na Papaso la Burudani, mmoja wa wasanii wa kundi hilo, Joh Makini, alisema kuwa ni miezi saba imepita toka Weusi watoe wimbo wa pamoja, hivyo mashabiki wana hamu ya kuwaona na kuwasikia, kupitia kolabo hiyo na Sauti Sol itakata kiu yao.

“G Nako anafanya poa na Alosto, Nikki anasumbua na Sweet Mangi na mimi pia Perfect Combo inafanya vizuri,  ila kuna ladha fulani ambayo mashabiki wanaikosa kutoka kundi la Weusi, nadhani kolabo hii itakuwa na jibu tosha kwa mashabiki wetu,” alisema Joh Makini, aliyekataa kutaja jina la wimbo huo mpya.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*