Kocha wa viungo Simba kutimka

NA ZAINAB IDDY

KOCHA wa viungo wa timu ya Simba, Adel Zrane,  raia wa Tunisia ameomba siku 10  za kwenda kupumzika nchini kwake.

Zrane anatarajiwa kuondoka muda wowote kuanzia sasa, baada ya kuomba ruhusa kwa uongozi wa timu hiyo, kwenda kushughulikia mambo ya kifamilia.

Akizungumza na BINGWA jana, Zrane, alisema ameomba kusafiri  kwa sababu muda huu Simba haina mechi yoyote hadi Januari, mwakani.

“Nimeomba ruhusa  niende nyumbani mara moja kuna masuala ya familia nimeruhusiwa nitaondoka muda si mrefu na nitarudi kabla ya Desemba 20,” alisema Zrane.

Kuondoka kwa Zrane kunaendelea kulifanya benchi la ufundi  kupungukiwa na watu baada ya kocha mkuu Patrick Aussems kuvunjiwa mkataba wake.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*