KOCHA UFARANSA APEWA UWANJA

PARIS, UFARANSA


 

KOCHA wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps, amepewa heshima kubwa baada ya jina lake kutumika kwenye uwanja mpya.

Kocha huyo ameandika historia kubwa kwenye soka nchini humo kwa kutwaa taji la Kombe la Dunia mwaka 1998 akiwa mchezaji na mwaka huu  akiwa kocha wa mabingwa hao.

Kutokana na mchango wake mkubwa wa mafanikio ya soka la nchini Ufaransa, hivyo amepewa heshima kubwa ya jina lake kutumika kati ya kiwanja kikubwa cha soka, hivyo kiwanja hicho kwa sasa kinajulikana kwa jina la ‘Stade Didier Deschamps’.

Hafla hiyo ilifanyika juzi kwenye uwanja huo mbele ya mashabiki 500, huku kocha huyo akiambatana na mke wake, Claude pamoja na mtoto wao, Dylan.

“Kwa upande wangu pamoja na familia ni heshima kubwa sana, jina la familia yangu kutumika kwenye uwanja ina maana kubwa sana.

“Kitu muhimu kwangu ni kuona vijana wenye umri mdogo wakifurahia jambo hili, wengine wamekuwa na furaha hadi wanadondosha chozi, hiyo ni sehemu ya furaha hakuna la zaidi,” alisema kocha huyo.

Deschamps amekuwa akiiongoza Ufaransa tangu mwaka 2021, lakini amekuwa na mafanikio makubwa sana na timu hiyo na kumfanya awindwe na timu mbalimbali duniani, lakini kutokana na mafanikio yake, shirikisho la soka nchini humo liliona bora wamwongezee mkataba mpya, hivyo mkataba wake wa sasa unatarajia kumalizika mara baada ya michuano ya Euro 2020.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*