googleAds

Kocha Toto Africans: Yanga imetupa uimara

NA DAMIAN MASYENENE, MWANZA

LICHA ya kuchapwa na Yanga mabao 3-0 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza, Kocha wa Toto Africans, Ibrahim Mulumba, amesema wachezaji wake wamepata uimara wa kupambana.

Akizungumza na BINGWA mara baada ya mchezo huo, Mulumba alisema mchezo huo  umesaidia kuwajenga uzoefu wachezaji wake wanaojiandaa na Ligi Daraja la Pili Tanzania Bara (SDL).

Mulumba alisema licha ya kufungwa, lakini mchezo huo ulikuwa ni  muhimu kwao katika maandalizi yao, kwani hadi sasa wamecheza michezo mitano ya kirafiki.

Alisema wamepanga kucheza mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya Gwambina inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara, baada ya kucheza na Mbao, Pamba na Alliance na Yanga.

 “Tunawashukuru Wanayanga Mkoa wa Mwanza kwa kuileta Yanga na kutukumbuka (Toto), mchezo huu ni muhimu kwani tunatafuta ufiti wa kupambana, uzoefu wa kucheza na timu kubwa na kurekebisha makosa madogo.

“Tulijitahidi kuwaheshimu kwa sababu ni timu kubwa na tumefurahia kuipata hii mechi imekuwa kipimo kizuri kwetu, tunaamini itatusaidia katika maandalizi yetu ya SDL,” alisema Mulumba.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*