googleAds

Kocha Stand: Wachezaji wangu wanabweteka

NA GLORY MLAY

LICHA ya Stand United kushinda mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara dhidi ya Sahare All Stars, kocha wa timu hiyo, Ally Mngazija,  amesema wachezaji wake wanabweteka mapema.

 Stand United  iliibuka huo katika mchezo uliochezwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.

Akizungumza na BINGWA juzi, Mngazija alisema wachezaji wake wangepambana vilivyo wangekufunga mabao mengi zaidi katika mchezo huo.

 “Wachezaji wangu inafikia wakati wanadharau mchezo, tunakuwa tunaanza kwa kasi kipindi cha kwanza, baadaye wanabweteka,” alisema Mngazija.

Stand United inapigania kurejea Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao baada ya kushuka daraja msimu uliopita kutokana na kufanya vibaya baadhi ya michezo yake.

@@@@@


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*