Kocha Singida United atamba hawatawaacha salama Namfua

NA WINFRIDA MTOI                                            

KOCHA wa Singida United, Ramadhan Nsanzurwimo, amesema baada ya kurejea kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Namfua, hawatakubali kufungwa.

 Kwa muda mrefu Singida United ilikuwa inatumia  Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha,  baada ya Bodi ya Ligi  kuufungia ule wa Namfua kutokana na kukosa sifa ya kuchezea Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano  mingine.

Akizungumza na BINGWA jana, Nsanzurwimo  alisema ana furaha kurudi  kwenye  uwanja wao wa  nyumbani kwa kuwa watakuwa wanacheza mbele ya mashabiki wao.

“Tumerudi nyumbani, tumeshinda bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting, naomba mashabiki watupokee na kutupa sapoti kubwa, nina uhakika tutafanya vizuri,” alisema Nsanzurwimo.

Alisema usajili aliofanya wa kuongeza wachezaji wapya wenye uzoefu, unatosha kabisa kukifanya kikosi hicho kuonesha ushindani katika michezo ya Ligi Kuu Bara.

Tayari Singida United imewasajili  Haruna Moshi ‘Boban’, Athuman Idd ‘Chuji’,  Ame Ali na Muharami Issa “Marcelo”  waliomtwaa kwa mkopo Yanga.

@@@@@@@@@


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*