KOCHA SIMBA AMWONDOA FEISAL YANGA

NA ZAINAB IDDY

ALIYEWAHI kuwa kocha na mchezaji wa zamani wa Simba, Abdallah Kibadeni, amesema anahesabu siku kwa kiungo wa Yanga, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’, kuendelea kuwepo ndani ya kikosi hicho kutokana na kiwango bora alichonacho.

Kibadeni ameliambia BINGWA jana kuwa msimu huu kwa wachezaji hususan nafasi ya kiungo, Feisal ameonekana kuwa bora zaidi ya wengine, licha ya uchanga alionao katika mikikimikiki ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Feisal ni kijana mdogo na ana kipaji cha mpira, iwapo kama hatashawishika na wenzake kuingia katika ujana, sidhani kama atakuwa na maisha marefu ndani ya Yanga kabla ya kupata nafasi nje ya Tanzania kucheza soka la kulipwa.

“Kijana huyu naweza kumfananisha na Simon Msuva, Shaban Chilunda pamoja na Farid Mussa, wameanza mpira wadogo, lakini wamejituma na mafanikio yake tumeyaona hivyo hata yeye siku si nyingi atapata mafanikio makubwa kupitia soka,” alisema.

Kibadeni aliongeza: “Jambo la msingi hivi sasa ni yeye kupunguza utoto na kutambua uwezo alionao, kisha kuufanyia kazi kwa kuweka malengo yatakayomfikisha mbali.”


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*