googleAds

Kocha Ruvu Shooting aivimbia Yanga


NA JESSCA NANGAWE

WAKATI Ruvu Shooting ikiisubiri Simba mwishoni mwa juma hili, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Salum Mayanga amesema kilichoitokea Yanga ndio kitawakuta wapinzani wao.

Simba na Ruvu Shooting zinatarajia kukutana mwishoni mwa juma hili kwenye uwanja wa Uhuru, ikiwa ni mwendelezo wa Ligi Kuu Tanzania bara baada ya mapumziko mafupi.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Mayanga alisema, kikosi chake kinajifua vilivyo kuweza kuwakabili wapinzani wao wakiwatahadharisha wasitegemee ushindi zaidi ya kukumbana na kipigo kama ilivyokua kwa Yanga walionyukwa bao 1-0.

Alisema hawana majeruhi huku wachezaji wake wakiwa na morali ya hali ya juu, hivyo hawana sababu yoyote ya kushindwa kupata matokeo mazuri.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*