KOCHA MPYA PSG AMCHIMBA MKWARA NEYMAR

PARIS, Ufaransa


KOCHA mpya wa klabu ya Paris Saint-Germain, Thomas Tuchel, ameanza na mkwara mzito ukianzia kwa straika wa timu hiyo, Neymar, akisema kuwa ni kama ‘msanii’na hatapewa upendeleo maalumu.

Kwa sasa hatima ya Mbrazil huyo ipo njiapanda baada ya wiki za hivi karibuni kuwapo tetesi zinazodai ataondoka licha ya kuwa si kipindi kirefu asajiliwe kwa bei mbaya ya Euro milioni 222 akitokea Barcelona, Agosti mwaka jana.

Real Madrid ndiyo inayodaiwa kumpa ofa Neymar ili aweze kurejea LaLiga, lakini Tuchel alisema juzi anatarajia atafanya kazi na straika huyo.

“Kwa maoni yangu mchezaji mkubwa ni yule ambaye    anafanya makubwa,” alisema Mjerumani huyo mara baada ya kutambulishwa. “Na katika yote huwa siogopi kufanya kazi na mastaa.  Nilikutana na Neymar Jumapili iliyopita na kilikuwa ni kikao muhimu. Ni msanii, ni mmoja kati ya wachezaji bora duniani, ni mchezaji muhimu wa kushinda mechi zetu.    Nilikipenda kikao chetu. Niliona kama usoni anatabasamu,”  aliongeza kocha huyo.

Alisema wachezaji wengine watakuwa naye watajenga taswira ya kile ambacho anataka wafanye.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*