googleAds

KOCHA MBEYA CITY ATAKA POINTI KWA AZAM

NA SAADA SALIM

Kocha Mkuu wa Mbeya City, Ramadhani Nsanzurwimo, amesema atahakikisha anaondoka na ushindi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam, utakaochezwa keshokutwa katika Uwanja wa Azam Complex, Dar e Salaam.

Akizungumza na BINGWA juzi Nsanzurwimo, alisema kikosi chake kipo tayari kwa mapambano licha ya kwamba watakuwa ugenini kuikabili timu inayowasumbua mara kwa mara, watahakikisha wanapata matokeo mazuri.

“Azam ni timu ngumu ambayo imekuwa ikitusumbua sana, lakini nikuambie tu kwamba tumejipanga vizuri kuhakikisha tunapata matokeo mazuri licha ya kwamba tutakuwa Uwanja wa ugenini,” alisema.

Msimu uliopita Mbeya City, walimaliza nafasi ya 12 na sasa kocha wao huyo amesema msimu huu ujao, watahakikisha wanamaliza nafasi za juu na kuepuka kuwa na presha ya kushuka daraja.

Azam wataingia uwanjani wakitokea Uganda ambao waliweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya utakaoanza kesho.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*