googleAds

Kocha Harambee Stars awaza mechi ya ufunguzi

CAIRO, Misri 

KOCHA mkuu wa Harambee Stars ya Kenya, Sebastien Migne, amesema lazima wachezaji wake wajiandae kimwili na kutuliza akili yao katika mechi ya ufunguzi AFCON dhidi ya Algeria itakayochezwa Jumapili katika Uwanja wa June 30 jijini Cairo, Misri. 

Kocha huyo raia wa Ufaransa alisema Harambee Stars watawacha kumbukumbu katika michuano hiyo mikubwa Afrika endapo watatumia vyema nafasi ambazo watazitengeneza.

Harambee Stars wapo Kundi C pamoja na Algeria, Senegal na Taifa Stars ya Tanzania.

“Tulikua na mchezo mzuri wa kirafiki dhidi ya DR Congo na kilichonifurahisha ni timu kujiamini na nadhani tulikuwa wazuri kuwazidi Congo lakini mwisho wa siku tukaambulia sare,” alisema Migne.

“Ilikuwa somo nzuri kwa wachezaji wangu kwamba wasisahau unapocheza na timu kubwa, chochote kinaweza kutokea na lazima tuwe makini hadi dakika ya mwisho, na pia unapopata nafasi ya kumaliza mchezo, fanya hivyo la sivyo soka inaweza kuwa hatari kwako.” 

Migne pia alitetea uamuzi wa timu kuweka kambi nchini Ufaransa akisema ilikuwa uamuzi bora kwa wachezaji ili waelekeze mawazo yao na kujiweka tayari kwa michuano hiyo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*