KOCHA AELEZA CHANZO MABONDIA KUCHEMSHA MADOLA

NA GLORY MLAY

KOCHA wa timu ya Taifa ya ngumi hapa nchini ambaye ni raia wa Kenya, Moses Oyombi, amesema mabondia wa Tanzania wanahitaji kucheza mapambano mengi ya kimataifa ili kujijengea uwezo zaidi.

Akizungumza na BINGWA jana, Oyombi, alisema changamoto ya kukosa mapambano ni chanzo cha kushindwa kimataifa, kwani kwa kucheza na mabondia wazoefu watajijenga na kuimarisha viwango vyao.

“Moja ya sababu zilizowafanya mabondia wa Tanzania kushindwa kutamba katika michuano ya Jumuiya ya Madola, ni kutokana na kukosa uzoefu wa mapambano ya kimataifa.

“Kwa kupanda ulingoni na mabondia wa ndani pekee haitoshi, hivyo wanahitaji kupata mapambano ya kimataifa ili kupima viwango vyao na kujiridhisha na uwezo wao wa kukabiliana na mabondia wa timu za nje,” alisema.

Hata hivyo, Oyombi alieleza kuwa viongozi bado wana kazi kubwa ya kuwapika mabondia hao ili waweze kuliletea taifa heshima kupitia mchezo wa ngumi.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*