Klopp: Mkizidi kunifurahisha nitawakumbatia mpaka basi

MERSEYSIDE, Liverpool

KOCHA wa timu ya Liverpool, Jurgen Klopp, amewapasha wachezaji wake kwa kuwaambia kwamba kama wanataka kuuona upendo wake kwao, basi hawana budi kupambana uwanjani na kumpa raha.

Bosi huyo wa majogoo hao wa jiji alionekana ni mwenye Furaha, huku akiwakumbatia wachezaji wake mara baada ya kumaliza mchezo wao wa ligi dhidi ya Chelsea kwa ushindi wa mabao 2-1.

“Haina umuhimu kwa watu kuniona na furaha na kuwakumbatia wachezaji wangu, lakini mimi nina furahia zaidi.

“Ni rahisi kwangu kuwakumbatia kwa furaha kutokana na upambanaji wao hadi tone la mwisho la mafuta kwenye mashine zao,” alisema.

“Sasa, kukiwa na kitu kama hiki katika chumba cha kubadilishia nguo na kuwaona wote wakiwa wanatabasamu, ni jambo zuri sana,” alimalizia Klopp.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*