Klopp aunga mkono mastaa Bayern kutoswa Ujerumani

LONDON, England

KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp, ameunga mkono uamuzi wa mwenzake wa kikosi cha timu ya Taifa ya Ujerumani, Joachim Low, kuwatema nyota watatu wa timu ya Bayern Munich, lakini akasema kwamba anatarajia vinara hao watamjibu.

Kauli hiyo ya Klopp imekuja baada ya mapema wiki iliyopita, Low kuwaondoa kikosini kwake, Thomas Muller, Jerome Boateng na Mats Hummels alichokitangaza kwa ajili ya mechi za kirafiki zijazo dhidi ya Serbia na Uholanzi.

Akizungumza juzi, Klopp ambaye kikosi chake usiku wa kuamkia leo kilikuwa kikiumana na Bayern katika mchezo wa marudiano katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora, alisema kwamba anafahamu vyema hatua hiyo ya Low.

“Hii inawezakana. Ila sifahamu mmoja kati yao hao watatu atakuwa anafahamu ni kwanini wametemwa,” kocha huyo aliuambia mkutano wa waandishi wa habari.

“Namfahamu Mats katika uzoefu wangu ni lazima atarudisha majibu. Kwa sasa wapo mapumziko katika timu ya taifa na watakuwa na nguvu zaidi,” aliongeza kocha huyo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*