FELLAINI AMVAA CARRAGHER

LONDON, England

KIUNGO wa Manchester United, Marouane Fellaini, amemvaa nyota wa zamani Liverpool, Jamie Carragher, akihoji alipotoa mamlaka ya kumkosoa wakati anakabiliwa na sakata la kumtemea mate mtu.

Carragher alisimamishwa kuchambua soka katika televisheni, baada ya kunaswa na kamera akimtemea mtu ambaye walionekana kutofautiana lugha.

Akizungumza juzi kuhusu maoni ambayo yaliwahi kutolewa na Carragher katika moja ya makala zake alizowahi kuandika juu yake, Fellaini alisema kwamba, alimshangaa sana staa huyo wa zamani na huku akimueleza kuwa ni mtu wa kutoa maneno bila kujiangalia mwenyewe.

“Ni kwa jinsi gani mtu kama Carragher anaweza kunifundisha ?” Fellaini aliliambia jarida la Sport/Voetbal.

“Huyu mtu ambaye alimtemea mate msichana akiwa ndani ya gari lake baada ya mechi dhidi ya Manchester United dhidi ya Liverpool. Sioni anachoweza kunifundisha,” aliongeza staa huyo.

Hata hivyo, alisema kwamba, kukosolewa ni kitu ambacho huwa kinamjenga mtu na ambacho pia humfanya ajitume zaidi ili kuwaonesha kuwa walikuwa wanakosea.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*