googleAds

Kiungo Liverpool aukataa ubingwa EPL

MERSEYSIDE, England

KIUNGO wa Liverpool, Georginio Wijnaldum, dizani fulani kama ameukataa ubingwa wa Ligi Kuu England hivi, licha ya timu hiyo kushinda michezo nane ya kwanza na kuongoza katika msimamo kwa pointi 24.

Wijnaldum raia wa Uholanzi alidai bado wana safari ndefu ya kukamilisha ndoto yao ya ubingwa ambao hawajawahi kushinda tangu msimu wa 1989/90.

“Bado hatujawa mabingwa, michezo 30 imebaki ambayo inabidi tupambane kwa jasho na damu, upinzani ni mkubwa, kila mmoja anatuangalia sisi,” alisema.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*