googleAds

KIUNGO ANAYEWANIWA YANGA AITAJA SIMBA

NA ESTHER GEORGE


KIUNGO wa Mbeya City anayewaniwa na Yanga, Kenny Ally, ameitaja Simba kama timu iliyowasumbua zaidi kwenye mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika mchezo baina ya timu hizo, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mbeya City.

Akizungumza na BINGWA jana, Kenny alisema mchezo kati yao na Wekundu hao ndio ulikuwa mgumu zaidi kutokana na ubora wa wapinzani wao.

“Simba walitupa wakati mgumu sana, tulipambana lakini mwisho wa siku wakatufunga, tunajipanga upya ili tutakaporudi mzunguko wa pili tuweze kufanya vizuri zaidi,” alisema Kenny.

Kiungo huyo anatajwa kuwaniwa na Yanga ambayo inataka kuimarika eneo la kiungo wa ukabaji ambalo kwa mujibu wa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Hans van der Pluijm, limekuwa likipwaya.

Xxxxxxxxxxxx


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*