googleAds

KISIGA AMTAJA ‘KIRUSI’ ANAYEINYIMA SIMBA MATAJI

NA WINFRIDA MTOI,

KIUNGO wa zamani wa Simba, Shaaban Kisiga, amefichua kile kinachoimaliza timu hiyo kuwa ni ukosefu wa mchezaji kiongozi kwenye kikosi hicho tofauti na watani zao Yanga.

Akizungumza na BINGWA juzi, Kisiga ambaye kwa sasa anaichezea Ruvu Shooting, alisema Simba ni timu nzuri iliyosheheni nyota wengi lakini inakosa wachezaji  wazoefu wenye uwezo wa kuwaongoza wenzao katika mambo mbalimbali ndani na nje ya uwanja.

“Simba inakosa mchezaji mwenye uwezo wa kuwaongoza wenzake na ambaye anaweza kusema kitu akasikilizwa, kama pale Yanga kuna ‘Cannavaro’ (Nadir Haroub).

Lazima awepo mchezaji mwenye uzoefu wa kutambua mambo na kusikilizwa ili  tatizo linapotokea awe mwenye uwezo wa kulitatua kabla halijaleta madhara,” alisema Kisiga.

“Pale Simba kila mchezaji ni staa ila linapokuja suala la uzoefu hawana. Kwa kawaida timu inatakiwa iwe na wachezaji wachache wazoefu kama wanavyofanya Yanga, matatizo yanatokea lakini silaha kubwa ni busara ya wachezaji,” alisema Kisiga.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*