googleAds

KLOPP ATAMBA KUITUNGUA CHELSEA DARAJANI LEO

LONDON, England


 

UNAKUMBUKA kile alichokifanya Eden Hazard juzi katika Uwanja wa Anfield? Basi Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, hataki kuona hilo likitokea leo wanapokutana na Chelsea ndani ya Stamford Bridge.

Mchezo uliozikutanisha timu hizo hivi karibuni katika michuano ya Kombe la Carabao ulimalizika kwa Chelsea kupata ushindi wa mabao 2-1 na kuwaondoa wenyeji wao kwenye michuano hiyo.

Kuelekea katika mchezo huo, Klopp ametamba kutumia silaha zake zote ili kusaka matokeo ya ushindi na kuendeleza rekodi ya kutokufungwa mpaka sasa ndani ya Ligi Kuu England.

Kocha wa Chelsea, Maurizio Sarri, naye yupo tayari kuharibu rekodi ya Liverpool na kuwashusha kileleni mwa Ligi Kuu England, ikiwa tayari amefanikiwa kuwaondoa katika Kombe la Ligi.

“Chelsea wapo vizuri kuanzia kwa wachezaji na kocha wao, tunahitaji kushinda dhidi yao, naamini tunayo nafasi ya kufanya hivyo, bila kujali kama tutakuwa ugenini,” alisema Klopp.

“Liverpool wapo vizuri, tukicheza kwa ushirikiano mzuri tunaweza kupata ushindi na kuwapa furaha mashabiki wetu watakaokusanyika Stamford Bridge, wote tupo tayari kuonyesha viwango vya juu kuibeba timu,” alisema Hazard.

Liverpool wanaongoza Ligi Kuu England baada ya kushinda michezo yote sita, huku wakifuatiwa kwa karibu na Chelsea, waliofanikiwa kushinda mitano na sare moja.

@@@@@@

Nyota Man United wamkazia Mourinho

MANCHESTER, England

IMERIPOTIWA kuwa kuna moto umewaka katika klabu ya Manchester United, kwani baadhi ya nyota wamekasirishwa na tabia ya Jose Mourinho kuwadhalilisha wenzao.

Baada ya kutolewa kwa mikwaju ya penalti na Derby katika michuano ya Kombe la Carabao, Mourinho aliwatupia maneno makali Phil Jones aliyekosa penalti na Eric Bailly.

Alisema hivi: “Nilijua tu kuwa tunakwenda kupata tabu tukiwa na Jones na Eric. Nililijua hilo mapema.”

Kauli hiyo, ambayo ilitanguliwa na nyingine ya Mourinho kumwambia Paul Pogba hatakuwa tena nahodha, imetajwa kuwachefua nyota wengine kikosini.

Hata hivyo, ingawa hatua watakazozichukua hazijawekwa wazi, huenda ikawa ni pamoja na kucheza ovyo katika michezo yao ijayo kwa lengo la kumfukuzisha kazi Mourinho.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*