KISA VIDEO CHAFU, NANDY ACHAFUA MITANDAO

NA MEMORISE RICHARD

MASHABIKI wa msanii wa Bongo Fleva Faustina Charles ‘Nandy’, hawajamwacha salama mrembo huyo baada ya jana kusambaa mtandao video chafu, inayomwonyesha akiwa katika mazingira ya faragha juu ya kifua cha rapa Billnas.

Katika siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Billnas hapo juzi Nandy aliweka picha yao tata kwenye ukurasa wake wa Instagram  na Papaso la Burudani lilipomuuliza kuhusu ukaribu wao alisema walikuwa studio wakirekodi wimbo wao mpya.

Nandy na Billnas wamekuwa wakikanusha kuwapo kwenye uhusiano wa kimapenzi mara kwa mara licha ya viashiria kadhaa kuonyesha wawili hao ni wapenzi mpaka jana ilipovuja video hiyo iliyochafua mitandao ya kijamii kwa mashabiki kumtukana mrembo huyo kwa kukosa heshima na kujidhalilisha katika video hiyo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*