googleAds

Kipa Simba ageuka Mkulima

NA MWAMVITA MTANDA

KIPA wa zamani wa Simba na Yanga,Deogratius Munishi, Dida amezua mjadala kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutupia picha tofauti zikimuonyesha akiwa shambani akilima.

Dida ambaye pia ni kipa wa zamani wa Azam FC,aliandika ujumbe mfupi usemao ndani ya Kilema masahera kati mkulima hachagui jembe.
Dakika chache baada ya kutupia picha hizo baadhi ya watu mbalimbali walimpongeza kwa uamuzi wake wa kujikita kwenye kilimo na kumpa moyo kuwa kitamtoa.

Wachangiaji wengine walionekana kumsikitia kwa uamuzi wake huo kwani ni kama amefulia kwa kijana kama yeye kuacha soka na kujikita kwenye kilimo huku damu ikiwa bado inachemka ya kukaa langoni.

“Novath Myinga aliandika “Hongera sana kaka wakati mwingine unakumbushia enzi japo kwa kushika jembe pekee cyo mbaya maana mguu.

DIMBA lilimvutia waya nyota huyo ili kufahamu kama ameamua kuchana kabisa na soka na kuhamia kwenye kilimo alisema, kwa muda huu ambao hana timu amemua kujikita kwenye kilimo kwani amekundua ndio kazi pekee ambayo inaweza kumsaidia katika maisha yake.

Kuna maisha baada ya mpira, bado ni ndoto za kucheza lakini kilimo ndio kila kitu kwa sasa,naweza kulima na nikacheza pia,îalisema Dida.

Hata hivyo Nyota huyo alisema, amepokea taarifa za kuitwa ndani ya timu ya taifa ya soka la ufukweni, lakini ameshindwa kwa kuwa anahitajika Boroka FC ya Afrika Kusini kwa ajili ya majaribio.

Muda wowote kuanzia sasa naweza kwenda Afrika ya Kusini,


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*