googleAds

Kipa RB Leipzig si kwa majigambo hayo

BERLIN, Ujerumani

MLINDA mlango wa RB Leipzig, Peter Gulacsi, amewatambia wapinzani akiwataka kujiandaa kwa vipigo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Union Berlin wikiendi iliyopita.

Gulasci, amesema hawana hofu hata kama watacheza na wababe wa ligi hiyo, Bayern Munich na Borussia Dortmund.

“Timu yetu ni changa kila mtu anafahamu, msimu uliopita tulikuwa na kiwango bora, tunataka kuendeleza makali yetu, hivyo wapinzani wajipange,” alisema Gulasci.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*