Kipa mkongwe Liverpool ampa tano Romero

MERSEYSIDE, Liverpool 

KIPA wa zamani wa Liverpool, David James, anaamini uwezo wa kipa wa Manchester United, Sergio Romero, hauna tofauti na Alisson.

Romero atasimama langoni kuchukua nafasi ya David de Gea ambaye anauguza majeruhi aliyopata akiwa kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Hispania.

“De Gea ni namba moja bila shaka, lakini nikimwangalia Romero tangu alipojiunga Man United, amekuwa na kiwango kizuri hadi sasa, hana tofauti na Alisson wa Liverpool, uwezo wao upo sawa tu,” alisema James.

Kesho timu hizo zitashuka dimbani Old Trafford kumenyana katika mchezo wa Ligi Kuu England unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*