Kipa Man United afungiwa mechi sita

MANCHESTER, England

KIPA wa Manchester United, Kieran O’Hara ambaye anaitumikia kwa mkopo Burton Albion amefungiwa michezo sita kwa kosa la kumpiga mchezaji wa timu pinzani.

Pia, kipa huyo raia wa Jamhuri ya Ireland, mwenye umri wa miaka 23 amepigwa faini ya pauni 2,500 kwa kosa hilo ambalo lilitokea dakika ya 44 walipocheza dhidi ya Peterborough.

O’Hara alikwepa adhabu ya mwamuzi uwanjani sababu ni tukio ambalo halikuonekana katika mchezo huo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Hata hivyo, Chama cha Soka England, FA, kiliandika taarifa ya kumfungia kipa huyo, baada ya kupitia picha za video na kugundua kosa hilo.

Mlinda mlango huyo ataanza kuitumikia adhabu hiyo katika mchezo ujao ambao wanatarajiwa kukutana na Lincoln City, pia, anatarajiwa kuonekana uwanjani mwezi ujao.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*