Kipa bora SportPesa achekelea kuitwa Stars

NA WINFRIDA MTOI MLINDA

MLINDA mlango wa Mbao FC, Metacha Mnata, ambaye aliibuka kipa bora wa michuano ya SportPesa, amesema alijisikia furaha jina lake lilipotajwa katika kikosi cha timu ya Taifa Tanzania, Taifa Stars, kwa kuwa ni ndoto zake za muda mrefu.

Mnata ni mchezaji aliyelelewa katika kituo cha Azam FC kama ilivyokuwa kwa Aishi Manula wa Simba, ambaye ndiye mlinda mlango namba moja wa Taifa Stars.

Akizungumza na BINGWA jana, Metacha alisema kuitwa timu ya Taifa ni moja ya fursa na hatua mojawapo katika maendeleo ya soka lake,  kwasababu inaonyesha jinsi  kazi yake ilivyoaminika.

“Namshukuru Mungu kuwa miongoni mwa wachezaji wanaounda timu ya Taifa, hiki ni kitu kikubwa kwangu na nitajituma na endapo nitapata nafasi nitadhihirisha uwezo wangu katika kuisaidia timu yetu,” alisema Metacha.

“Kila mchezaji anakuwa na ndoto ya kucheza timu ya Taifa, kama nilivyojituma kuisaidia timu yangu ya Mbao katika michuano ya SportsPesa na kufanikiwa kuwa kipa bora, hata Taifa Stars nikipata nafasi nitafanya hivyo,” aliongeza Metacha.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*