googleAds

KIPA AFRICAN LYON AMSHANGAA MSUVA

NA JESSCA NANGAWE,

KIPA namba moja wa African Lyon, Youthe Rostand, amemshangaa winga wa Yanga, Simon Msuva, kuendelea kucheza Bongo wakati ana hadhi ya kucheza Ulaya.

Akizungumza na BINGWA, Rostand ambaye anadaiwa kuivutia Yanga na huenda akatua katika klabu hiyo msimu ujao, anaamini huu ni wakati wa Msuva kutimkia Ulaya kama anataka kukuza zaidi kiwango chake.

“Tangu nije Tanzania nimeona mastraika wazuri sana, wana uwezo ambao mimi naona hawakupaswa kuwa hapa, walitakiwa wawe kwenye klabu kubwa kama anayocheza Samatta.

Kuna mchezaji wa Yanga anaongoza kwa magoli, Msuva mimi sioni kama alipaswa kuwa hapa, alitakiwa awe anacheza klabu kubwa kutokana na uwezo wake,” alisema kipa huyo.

Kipa huyo ambaye bado ana mkataba mwingine wa mwaka mmoja na Lyon, amezialika timu mbalimbali zinazohitaji huduma yake msimu ujao kukaa meza moja na uongozi wa klabu yake.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*