googleAds

King Kibadeni amchokoza Dk. Msolla

NA WINFRIDA MTOI

KUELEKEA pambano la watani wa jadi, nyota wa zamani wa Simba, amewataka wachezaji wa timu hiyo kuibuka na ushindi mnono dhidi ya Yanga ili kumpa raha mwekezaji wao, Mohammed Dewji ‘Mo’.

Kauli hiyo ya Mkwasa ni kama uchokozi kwa Mwenyekiti wa Yanga, Dk. Mshinso Msolla, viongozi wenzake na wapenzi wa klabu hiyo kwa ujumla.

Simba na Yanga zinatarajia kukutana Januari 4, mwaka huu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Kibadeni alizungumza hayo katika hafla ya wanachama na wapenzi wa timu hiyo ya kuonyeshwa Uwanja wa Bunju, Dar es Salaam, baada ya kukamilika.

Alisema mwekezaji huyo anafanya mambo makubwa na kujitoa kwa dhati kuisadia klabu hiyo kupiga hatuam hivyo ni jukumu la wachezaji kujituma na kujitoa uwanjani kwa kila mechi.

“Ni kitu kikubwa kimefanyika, haijawahi tokea kwa miaka yote, nawaomba wachezaji ili kurudisha fadhila ni kufanya vizuri, tena nataka mechi ijayo na Yanga tushinde, hii itakuwa furaha pekee kwa mwekezaji wetu,” alisema Kibadeni.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*