googleAds

KIBADENI: YANGA SC MASHUJAA

NA ZAINAB IDDY

KOCHA na mchezaji wa zamani wa Simba, Abdallah ‘King’ Kibadeni, ameipa tano klabu ya Yanga kutokana na kitendo cha kujitokeza hadharani kuomba msaada wa kifedha kwa wanachama na mashabiki wao, akikiita ni cha kishujaa.

Akizungumza na BINGWA jana, Kibadeni alisema viongozi wa Yanga wamefanya jambo kubwa na la kihistoria na linaweza kuwapa matunda mazuri na kuwa somo kwa klabu nyinginezo.

“Tumeona baadhi ya timu za Ligi Kuu na hata Ligi Daraja la Kwanza zikidai hazina uwezo wa kifedha, lakini hawajafanya tukio kama la Yanga.

“Unapoamua kuandaa tukio maalumu kwa ajili ya kuchangia kitu hata yule ambaye hakuwa tayari kuwachangia, anashawishika kuwasaidia, binafsi nawapongeza sana Yanga kwa hili,” alisema.

Kibadeni alisema: “Watanzania tumekuwa na kawaida ya kudharau kidogo na kukipa uzito kikubwa cha mara moja huku tukisahau kuwa kile tunachokiona si kitu, kina uwezo wa kuwa na uzito sawa na tunachokithamini.

“Timu nyingine zinapaswa kuwaiga Yanga, ninauhakika wanachama na mashabiki wana nguvu kubwa ya kuisaidia timu yao kuliko makampuni au taasisi ambazo nyingine zina masharti magumu,” alisema.

“Watanzania tumekuwa na kawaida ya kudharau kidogo na kukipa uzito kikubwa cha mara moja huku tukisahau kuwa kile tunachokiona si kitu, kina uwezo wa kuwa na uzito sawa na tunachokithamini.

“Timu nyingine zinapaswa kuwaiga Yanga, ninauhakika wanachama na mashabiki wana nguvu kubwa ya kuisaidia timu yao kuliko makampuni au taasisi ambazo nyingine zina masharti magumu,” alisema.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*