KHLOE KARDASHIAN: JAMANI NIACHENI NA MIMBA YANGU

NEW YORK, Marekani


 

STAA wa vipindi vya runinga ambaye pia ni mwanamitindo, Khloe Kardashian, amewakaribisha mashabiki kupata uzoefu wa safari yake ya ujauzito, lakini akawaomba kuelewa kwamba  mabadiliko yake ya kimwili yanaonekana zaidi kutokana na ujauzito huo.

Staa huyo alitoa kauli hiyo juzi kupitia ujumbe alioutuma kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram akitetea mwonekano wake wa sasa wakati akiandaa kipindi kingine cha runinga cha  Keeping Up With the Kardashians, ambacho kilianza kurushwa usiku wa kuamkia leo.

Mama huyo kijacho alisema kuwa hali hiyo ilimtokea pia wakati wa ujauzito  wa mwanawe mwingine wa kike, True Thompson na anakiri kwamba yeye pia anaichukia kutokana na kwamba anashindwa  kudhibiti juu ya mwonekano wake.

“Hali hii inasababishwa na ujauzito,” aliandika Khloe katika ukurasa huo. “Baadhi ya wanawake huwa wanakutana na hali kama hii na mimi ni mmoja wapo, maumbile yangu yanakuwa mabaya niamini mimi na hilo nalifahamu,” aliongeza staa huyo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*