Khadija Yusuph arudi kundini kuokoa Jahazi

NA JEREMIA ERNEST

MWANAMUZIKI nyota wa taarabu nchini, Khadija Yusuph, ameamua kurudi tena katika bendi pendwa ya muziki huo, Jahazi Modern Taarab ili kuiweka tena kwenye ramani kama ilivyokuwa zamani.

Akizungumza na Papaso la Burudani jana, Khadija alisema anarudi kundini kuiokoa bendi ya Jahazi ambayo imekuwa ikishuka kadiri siku zinavyokwenda toka mwasisi wake Mzee Yusuph aache muziki.

“Tumerudi katika bendi ya Jahazi ili kuiokoa na kuirudisha katika ubora ambao ulikuwa mwanzoni, sijarudi peke yangu nipo na waimbaji wengine na tutakuwa tunafanya shoo kila siku za Jumanne katika Ukumbi wa DDC Kariakoo,” alisema Khadija.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*