KHADIJA KOPA ARUKA DENI LA KAPTENI TEMBA

NA JEREMIA ERNEST


MALKIA wa Taarabu nchini, Khadija Kopa, amekanusha tuhuma za kudaiwa fedha za utunzi wa wimbo wa Mwanamke Jeuri na mtunzi wa nyimbo, Kapteni Temba, kama alivyotangaza katika mitandao ya kijamii.

Khadija Kopa amelipasha Papaso la Burudani kuwa, hajawahi kuandikiwa wimbo halafu asimlipe mtunzi hivyo Kapteni Komba aache kumchafua, kwani hajawahi kufanya naye kazi.

“Hajawahi kuniuzia wimbo, nashangaa ananichafua kwenye mitandao ya kijamii, kama ananidai aende polisi kama atakuwa na maandishi tuliyoandikishiana, sijazoea utapeli,” alisema Kopa.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*