KATOSWA UFARANSA WAMKANA ZIDANE

PARIS,   Ufaransa


RAIS wa Shirikisho la Soka Ufaransa (FFF), Noel Le Graet, amekana kocha wa zamani wa Real Madrid,  Zinedine Zidane, kupewa timu ya taifa na akasisitiza kuwa waliyenaye kwa sasa, Didier Deschamps, ataendelea kukinoa kikosi hicho hadi mwaka 2020.

Zidane alitangaza kuachia madaraka ghafla wiki iliyopita zikiwa ni siku chache tangu awawezeshe vinara hao wa soka Hispania kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Liverpool.

Tangu kipindi hicho, kocha huyo mwenye umri wa miaka 45, amekuwa akihusishwa kupewa mikoba hiyo ambayo inashikiliwa na mchezaji mwezake wa zamani, Deschamps, ambaye ameiwezesha Les Blues kutinga fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika hivi karibuni nchini Urusi.

Hata hivyo, jana Le Graet alisema staa huyo wa zamani ambaye aliwawezesha kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka 1998, hataweza kuinoa Ufaransa kabla ya mwaka 2020.

“Zidane kesho anaweza kusaini na Juventus,   ila sifahamu chochote,” Le Graet aliuambia mtandao wa RMC. “Mmenishangaza sana lakini siwezi kuanzisha mjadala kuhusu ‘Didier-Zizou’, jambo hilo si la kweli. Tutaanza fainali za Kombe la Dunia tukiwa na Didier. Kwani alisaini mkataba hadi mwaka  2020,”  aliongeza rais huyo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*