googleAds

Kaseja ajifua kivyake kumkabili Manula Stars

ZAINAB IDDY

KIPA Juma Kaseja ameendelea kujifua kivyake, licha ya kocha wa timu yake ya KMC,  Jackson Mayanja,  kuwapa mapumziko ya siku tatu, baada ya kurejea nchini wakitokea Kigali, Rwanda kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu Kombe la Kagame.

KMC iliyoshiriki kwa mara ya kwanza michuano ya Kagame ilishindwa kutinga robo fainali kutokana na kufanya vibaya hatua ya makundi.

Kaseja ni kati ya makipa watatu walioitwa katika kikosi cha Tanzania, Taifa Stars, kwa wachezaji wanacheza Ligi ya Ndani ya Nchi kujiandaa na mchezo wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Chan) dhidi ya Kenya, utakaochezwa Julai 28, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Makipa wengine walioitwa na kaimu kocha mkuu wa Taifa Stars, Etienne Ndayiragije ni Aishi Manula wa Simba naMetacha Mnata wa Yanga.

Akizungumza na BINGWA jana, Kaseja alisema haoni sababu ya kumpumzika kufanya mazoezi, licha ya kupewa siku za kupumzika, baada ya kazi kubwa waliyoifanya Rwanda.

“Kocha Mayanja ametoa mapumziko baada ya kutoka Rwanda katika michuano ya Kagame Cup, lakini sikuona umuhimu wa kupumzika  kutokana na jukumu kubwa linalonikabili kwa timu ya Taifa,” alisema

Kaseja kabla ya kutua KMC aliwahi kuzichezea timu za Moro United, Simba, Yanga,  Mbeya City na Kagera Sugar.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*