googleAds

Karia: Nguvu zote Stars kwa Sudan

NA TIMA SIKILO

RAIS wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Wallace Karia, amesema wameshaanza kuwafungia kazi Sudan kuelekea mchezo wa kutafuta tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) mwakani.

Stars walifanikiwa kuitoa Kenya kwa mikwaju ya penalti 4-1 katika hatua ya awali, baada ya timu hizo kutoka suluhu mechi zote mbili, nyumbani na ugenini.

Akizungumza na BINGWA jana, Karia alisema baada ya Stars kufanikiwa kutinga hatua ya makundi ya kuwania tiketi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia kwa kuitoa Burundi, kwa sasa hawapoi na akili zao zote zimeelekezwa Sudan.

Alisema tayari wameshaanza kufanya vikao vya kuona ni vipi Stars inaitoa Sudan na kuzidi kuchanja mbuga, huku azma yao ikiwa ni kushiriki fainali hizo.

Aliwapongeza wachezaji wote wa Stars kwa kujituma kwao, akiamini timu hiyo itaendelea kufanya vizuri na kufanikiwa kufuzu CHAN na hata kucheza Kombe la Dunia nchini Qatar 2022.

 “Sasa hivi tuna vikao vya kujipanga na mchezo wetu wa Sudan kwani ndio wapinzani wetu wanaofuata, tunahitaji kupata ushindi nyumbani na hata kwao,” alisema.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*