KANYE WEST AJICHONGEA TENA KWA MASHABIKI

NEW YORK, Marekani


RAPA Mahiri, Kanye West, amejichongea tena kwa mashabiki baada ya kuibuka mkutano na fulana yenye ujumbe wa kuwataka wapiga kura wenye asili ya Afrika kuachana na Chama cha  Democratic.

Staa huyo ambaye ni shabiki mkubwa wa Rais wa Marekani, Donald Trump, aliibua hasira hizo za mashabiki ambao walianza kumwandama na ujumbe mzito kupitia katika mtandao wake wa Istagram.

Katika ujumbe huo, baadhi ya mashabiki wake walieleza kuwa ndio maana wanampango wa kususia bidhaa zinazotengenezwa na kampuni yake.

“Ni kwanini tumwache aendelee na upuuzi wake huo, lazima tuchukue hatua,” ulieleza ujumbe mwingine.

“Kwanini anadhani watu weusi ni vipofu, kondoo au mabubu? Ninachukia jinsi wanavyoendelea kuifanya jumuiya ya watu weusi haiwezi kuwa na mawazo ya kujitegemea? Sisi hatumkubali Donald Trump kutokana na matendo yake ya kusikitisha na anawakilisha chama chake na watu wake. Hata kama maoni yao hayawezi kuwa sawa na yake, bado ni msemaji wao,” aliongeza shabiki huyo.

Hatua hiyo imekuja zikiwa ni wiki  chache baada ya rapa huyo kuibua maswali mengi kwa mashabiki kwa kujisifia kwamba, kofia aliyopewa na Rais Trump imemfanya kuwa mwanamume mwenye nguvu za ajabu.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*