KANE ATAMANI KUIONGOZA ENGLAND

LONDON, ENGLAND

STRAIKA wa timu ya Taifa ya England, Harry Kane, ameweka wazi kwamba, atakuwa na furaha kubwa endapo atapata nafasi ya kuwa nahodha wa timu hiyo kwenye fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi.

Kocha wa timu hiyo, Gareth Southgate, anatarajia kutangaza majembe yake Mei 15, ambayo atakwenda nayo nchini Urusi.

Kocha huyo tangu amechukua nafasi ya kuisimamia timu hiyo mwaka 2016, hakuwa na nahodha wa kudumu, lakini anaweza kumtaja nahodha mara baada ya kuita kikosi hicho.

“Kocha ameweka wazi kuwa, muda wowote anaweza kumtaja nahodha wa timu hiyo kuelekea Kombe la Dunia, hivyo kila mmoja anasubiri kusikia jina litakalotajwa.

“Hata hivyo, kwa upande wangu nitahakikisha ninafanya kazi yangu kama kawaida bila kujali ninakuwa nahodha au mchezaji wa kawaida, lakini kupata nafasi hiyo ni kitu ambacho nitajivunia.”

Alisema kwamba, pia anavyoamini, timu yao inaweza kuwa bora katika safu ya ushambuliaji na kuwafanya waweze kufunga mabao mengi.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*