Kanda aanza mazoezi mepesi

NA MWAMVITA MTANDA

WINGA wa timu ya Simba, Deo Kanda, amesema  ameanza mazoezi mepesi na muda si mrefu ataonekana uwanjani, baada ya kuumia katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga.

Kanda alipata jeraha la kifundo cha mguu katika mchezo huo, uliochezwa  Januari 4, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Akizungumza  na BINGWA jana, Kanda alisema anatarajiwa kuungana na wenzake wiki hii, kwa sasa anafanya mazoezi mepesi ya kujiweka fiti.

Kanda alisema “Nashukuru Mungu naendelea vizuri, japo ile siku nilipata maumivu makali sana, lakini naweza kutembea vizuri sasa, nitajiunga na wenzangu, lakini naweza kukosa mechi moja ya hivi karubuni,”alisema Kanda.

Alisema anaamini wachezaji wenzake wanafanya kazi nzuri, licha ya kukosekana kwake, kwani  hajaona pengo kubwa.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*