googleAds

KAMUSOKO BADO AIOTA MBEYA CITY

NA SAADA SALIM,

KIUNGO wa Yanga, Thabani Kamusoko  amesema amecheza mechi nyingi ngumu  msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini  amekiri kwa  Mbeya City ilikuwa zaidi.

Kamusoko alikuwa sehemu ya kikosi cha  Yanga ambacho wikiendi iliyopita kiliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City katika pambano la Ligi Kuu Tanzania Bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA, Kamusoko aliisifu Mbeya City akisema ni timu imara inayocheza soka la malengo.

“Nimecheza mechi nyingi lakini ile na Mbeya City ilikuwa ngumu sana kwetu, tulikuwa tunahitaji pointi tatu muhimu kujihakikishia taji letu la ubingwa.

Wapinzani wetu nao walikuwa makini sana kuhakikisha wanatuzuia,” alisema kiungo huyo raia wa Zimbabwe na kuongeza.

“Mechi ilikuwa ngumu zaidi baada ya wao kupata bao la kusawazisha na kuanza kutafuta kwa nguvu bao la pili, walicheza kwa umoja wa hali ya juu, lakini umakini wetu ulitusaidia tukapata ushindi.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*