googleAds

Kahata, Kagere ndani ya nyumba

NA JESSCA NANGAWE

NTOTA wa Simba, Francis Kahata na Medie Kagere, wanatarajia kuungana na wenzao kabla ya pambano lao dhidi ya Mtibwa Sugar litakalopigwa Ijumaa hii Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Simba na Mtibwa Sugar sasa zitamenyana keshokutwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam baada ya Bodi ya Ligi kupangua ratiba hiyo ambayo awali lilikua lipigwe Septemba 17.

Wachezaji hao walikua kwenye majukumu ya timu zao za taifa ambapo Kahata alikua na Harambe Stars huku Kagere akiwa na timu yake ya Amavubi ya Rwanda.

Kwa mujibu wa kocha, Patrick Aussems, wachezaji hao ni muhimu ndani ya kikosi chake na kwamba Kahata alitarajiwa kutua jana, huku Kagere yeye atawasili kesho.

“Kama unavyotuona, hapa ni wachezaji wawili pekee hawapo kutokana na majukumu ya timu za mataifa yao, Kahata anawasili leo (jana) jioni, Kagere yeye ni Alhamisi,” alisema.

Aliongeza kwasasa wachezaji karibu wote wako katika hali nzuri na wapo tayari kwa pambano hilo muhimu ambapo lengo lao ni kuhakikisha wanavuna ushindi muhimu wa pointi tatu.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*