googleAds

Kahata apata majanga

NA JESSCA NANGAWE

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Francis Kahata, amepata majanga na kurejea kwao nchini Kenya kutokana na kuuguliwa na mtoto wake.

Kahata aliyesajiliwa na Simba akitokea Gor Mahia ya Kenya, aliondoka nchini juzi baada ya kupewa ruhusa na uongozi wa klabu hiyo kwa ajli ya kwenda kushughulikia matibabu ya mwanaye huyo.

DIMBA Jumatani lilielezwa juu ya mkasa wa kiungo huyo ambaye anatarajiwa kurejea siku yoyote kutegemea na hali ya mgonjwa.

Kiongozi mmoja ndani ya klabu hiyo aliyekataa kutajwa jina lake kutokana kuwa siyo msemaji alikiri na kudai amewasiliana na baadhi ya wachezaji wenzake akisema hali ya mtoto wake kiasi inaridhisha.

“Ni kweli Kahata ameenda kwao kutokana na mwanaye kuugua, atarejea wakati wowote hali ikiwa sawa, kwa sasa ligi imesisima kidogo hivyo hatukuona sababu ya kumzuia kwenda kumuuguza mwanaye huyo,” alisema kiongozi huyo.

Inasemakana kiungo huyo anauguliwa na mwanaye wa kike aitwaye, Winsy Kahata, lakini haijafahamika mara moja anasumbuliwa na ugonjwa gani.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*