googleAds

Kagere, Niyonzima, Sibomana wafungiwa Rwanda

NA MWAMVITA MTANDA

WACHEZAJI wa kimataifa wa Rwanda wanaokipiga Ligi Kuu Tanzania Bara, Meddie Kagere wa Simba, Haruna Niyonzima na Patrick Sibomana (Yanga), wamezuiwa kutoka nje ya mpaka wa nchi yao hiyo kwa siku 14.

Nyota hao waliondoka nchini baada ya tamko la Serikali kusimamisha shughuli zote zinazohusu mikusanyiko ya watu, ikiwamo Ligi Kuu Bara kwa siku 30 kutoka na hofu ya virusi vya Corona.

Serikali ya Rwanda nayo imechukua tahadhari juu ya janga hilo jana, kwa kutangaza kupiga marufuku safari zote za kuingia na kutoka nchini humo kwa siku 14. 

Akizungumza na BINGWA jana kutoka Rwanda, Sibomana alisema ni jambo la kumuomba Mungu mpaka kufikia siku hizo 14 hali iwe shwari ili kila mmoja arudi kwenye majukumu yake.

“Siku 14 zitaisha kabla ya muda wetu tuliopewa haujafika, kama tumepewa siku 30 (Tanzania), basi tunaweza kurudi kazini, tunachoomba hali iwe shwari kote duniani,” alisema Sibomana.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*