googleAds

Kagere aweka rekodi tuzo ya mwezi VPL

NA JESSCA NANGAWE

KINARA wa mabao msimu uliopita, Meddie Kagere wa Simba, amechaguliwa tena kuwa mchezaji bora wa mwezi Agosti na kamati ya tuzo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kagere amefanikiwa kushinda tuzo hiyo na kuwabwaga wenzake Lucas Kikoti wa Namungo FC na Seif Karie kutoka Lipuli.

Mpaka sasa tayari Kagere ameisaidia timu yake kupata ushindi wa mabao 3-1 mbele ya JKT Tanzania huku akitupia mawili na lingine likifungwa na Miraji Athuman iliyotokana na pasi yake, mchezo uliopigwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Hii ni mara ya nne kwa Mnyarwanda huyo kushinda tuzo hii baada ya msimu uliopita kuibuka mara tatu; Agosti, Februari na Mei.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*