googleAds

KAGERA AOGA NOTI

NA SALMA MPELI

Straika wa kimataifa wa Simba, Meddie Kagere, juzi alioga noti baada ya kukabidhiwa kitita cha shilingi 150,000 kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo wa kundi la Simba Forever, kutokana na mchango wake mkubwa kwa timu hiyo.

Mchezaji huyo alikabidhiwa fedha hizo jana baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya African Lyon, uliopigwa juzi katika Uwanja wa Taifa na kumalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Kiongozi msaidizi wa kundi hilo, Dickson Kilambakime, alimkabidhi fedha hizo Kagere ambaye aliibuka mshindi wa mwezi Septemba akiwashinda wachezaji wenzake, Cletous Chama na Shomari Kapombe.

Baada ya kukabidhiwa fedha hizo, Kagere alisema anashukuru kwa Wanasimba kutambua mchango wake, zawadi hiyo itazidi kumwongezea morali wa kufanya vizuri katika mechi zijazo.

“Nashukuru sana, sikutegemea kitu kama hiki zawadi hii itaniongezea morali zaidi kwenye mechi nyingine za ligi inayoendelea na nawashukuru mashabiki wa Simba kwa kuitambua kazi yangu,” alisema Kagere.

Kundi hilo la Whatsapp la Simba Forever limejiwekea utaratibu wa kutoa zawadi ya fedha kwa mchezaji mmoja mmoja anayefanya vizuri katika mwezi husika ambako mara ya mwisho walimpa Hassan Dilunga.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*