KAGERE AMFUMBUA MACHO SHIME

NA ZAINAB IDDY

KITENDO cha mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere, kuifunga JKT Tanzania mabao mawili katika ushindi wa 2-0 walioupata Wekundu hao wa Msimbazi, ni kama kimemshtua kocha mkuu wa maafande hao, Bakari Shime.

Licha ya kucheza katika uwanja wao wa nyumbani wa Mkwakwani jijini Tanga, maafande hao wa JKT Tanzania hawakuweza kuhimili kasi ya Simba na kukubali kipigo hicho cha mabao 2-0 yote yakifungwa na Kagere.

Kagere aliifungia timu yake mabao hayo yote kipindi cha kwanza dakika ya 13 na 39,  hivyo kuvunja rekodi kwani tangu kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, JKT Tanzania wamecheza mechi 11 bila kufungwa mabao ya mapema.

Akizungumza na BINGWA, Shime alisema anachukizwa na wachezaji wake kukubali kufungwa mabao rahisi kama lile la kwanza walilofungwa na Simba, kwani hadi sasa linamuumiza na kumpa kazi ya kuzungumza na wachezaji wake mara kwa mara.

“Mchezo tumecheza wiki iliyopita lakini mara kwa mara ninapokaa na kutulia, lile bao la kwanza tulilofungwa limekuwa likijirudia rudia akilini kwangu, hii inaonyesha wazi hatukustahili kufungwa.

“Sipo tayari kuona tunafungwa mabao ya kizembe tena katika timu ninayofundisha na kama ikijitokeza tena, itanibidi nitafute njia mbadala ya kuzuia,” alisema.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*