Kado awashangaa makipa chipukizi

NA WINFRIDA MTOI

KIPA Mtibwa Sugar, Shaaban Kado, ameshangazwa na viwango vya makipa chipukizi wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu kutokana na ushindani mkubwa uliopo.

Akizungumza na BINGWA, Kado alisema makipa wachanga wanaonekana kuja juu na kuwapa ushindano wakongwe, kitu kinachomfurahisha na kuona wataacha warithi bora katika tasnia hiyo.

Kado alisema pamoja na makipa hao kuwa na ubora kuna vitu wanaendelea kuwaelekeza badhi ya kama wakongwe ili kuwaongezea umakini wanapokuwa langoni.

“Makipa wa chipukizi wako vizuri, tunawasapoti pale wanapohitaji msaada, ili waendelee kuwa bora zaidi kwa sababu soka kila siku linabadilika na ushindani unaongezeka,” alisema Kado.

Kado ni kati ya makipa wakongwe hapa nchini anayeendelea kufanya vizuri akiwa kipa namba moja wa Mtibwa, timu nyingine alizowahi kucheza ni Yanga na Azam.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*