Jux awatembelea majeruhi wa moto Morogoro

JEREMIA ERNEST

Mkali wa RnB nchini, Juma Musa ‘Jux’, mwishoni mwa wiki iliyopita, alitembelea eneo ilipotokea ajali ya moto mkoani Morogoro na kwenda hospitali wa mkoa huo kuwajulia hali waathirika wa tukio hilo.

Akizungumza na Papaso la Burudani jana, Jux alisema ameona vyema kuwajulia hali majeruhi hao na kutoa kidogo alichojaaliwa .

“Wengi walipata ajali hii ni vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa, nimekuja kuwapa moyo ambao walinusirika na kuwaombea warejee katika hali zao kwa haraka kama ilivyokuwa awali, ” alisema Jux aliyeongozana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Steven Kabwe.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*