JUX AIPELEKA AFRICAN BOY KIMATAIFA

NA CHRISTOPHER MSEKENA

NYOTA wa Bongo Fleva Juma Musa ‘Jux’ jana aliingia makubaliano na kiwanda cha Vendome kilichopo Guangzhou, China kwa ajili ya kuzalisha na kusambaza bidhaazake za African Boy.

Jux ambaye aliongozana na mpenzi wake Vanessa Mdee wiki hii walikuwa nchini China na tayari kusaini dili hizo litalofanya bidhaa za African Boy kama vile Kofia, fulana, mabegi na viatu kutengenezwa na kuuzwa kimataifa.

“Mwanzoni nilitaka kuonyesha kijana wa Afrika ambaye ni mchakarakiji na anayesoma nchini China lakini baadaye ikageuka na kuwa bidhaa, leo (jana) nimesaini dili la bidhaa zangu kutengenezwa hapa China na kusambazwa duniani,” alisema Jux.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*